Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA), Kanda ya Mashariki imebaini dosari mbalimbali kwenye maabara binafsi ambazo zinakiuka sheria.

Imeelezwa kuwa wamiliki wa maabara hizo wamekuwa wakifanya tohara bila kuzingatia taratibu za kiafya, kulaza wagonjwa pamoja na kutoa tiba na vipimo visivyostahili.

Dosari hizo zimebainika katika tathimini za ukaguzi zilizofanywa kwa miaka mitatu (2020/2021-2024/2025)
katika wilaya ya Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza.

Kufuatia halli hiyo Mamlaka hiyo imewataka wamiliki hao Mkoa wa Mwanza kutoangalia faida pekee wakati wanaangamiza watu na badala yake wazingatie sheria, kanuni na miongozo ya afya iliyowekwa na Serikali ili kulinda afya za watu.

✍️✍️Tausi Mbowe
#starTvupdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *