Serikali imeongeza juhudi katika mapambano dhidi ya dawa bandia ili kuhakikisha afya za wananchi zinalindwa.
Akizungumza katika kikao kazi baina ya Mamlaka ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi (TMDA), Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Matiko Chacha amesema Serikali itaendele kushirikiana na TMDA katika kudhibiti dawa hizo.
Ameongeza kuwa Serikali haitosita kuchukua hatua kali dhidi ya watu wote wasio waaminifu wanaojihusisha kusambaza na kuuza dawa bandia.
Awali washiriki wa kikao hicho wamesema watatumia mafunzo hayo waliyoyapata kuelimisha jamii umuhimu wa matumizi wa dawa sahihi.
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)