Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliwaambia wananchi wa Iran kwamba: Kwa kumpa adui pigo, mmemfahamisha kwamba hapambani tu na makombora, ndege zisizo na rubani, torpedo na zana za kijeshi pekee kwani mstari wa mbele wa Iran ni mpana sana kuliko taswira yake ndogo na iliyodhalilika.

Ayatullah Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo Ijumaakatika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa Kiirani wa  1405 Hijria Shamsia.

Amesema mwaka huu, majira ya kuchipua ya kiroho na ya kimaumbile , yaani Sikukuu Tukufu ya Idd al‑Fitr na sikukuu ya kale ya Nowruz,  zimekutana kwa wakati mmoja. Kwa mnasaba huu, amewapongeza wananchi wote kwa sikukuu hizi mbili za kidini na kitaifa, na pia amewapongeza Waislamu wote duniani kwa Idd al‑Fitr.

Katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu ameashiria  matukio matatu ya vita dhidi ya Iran katika mwaka uliopita wa Hijria Shamsia. Vita vya kwanza ni vita vya siku 12 vya mezi Juni mwaka jana vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kushirikiana na Marekani. Amesema adui alifanya kosa kubwa katika makadirio yake kwa kudhani  kwamba baada ya siku moja au mbili tu, wananchi hawa wenyewe wangesimama na kuuangusha mfumo wa Kiislamu. Hatimaye, kupitia upatanishi na juhudi za kusitisha mapigano, alijinasuasua na kujiepusha na hatari iliyokuwa ikimkabili.

Aidha ameashiria jaribio la mapinduzi dhidi ya mfumo wa Kiislamu nchini Iran mwezi Disemba, ambapo Marekani na utawala wa Kizayuni, wakidhani kuwa wananchi wa Iran, kutokana na matatizo ya kiuchumi ya kulazimishwa, wangeitikia matakwa ya adui. Maadui walitumia vibaraka wao na kusababisha maafa mengi. Katika tukio hilo, idadi kubwa zaidi ya wananchi wetu wapendwa walipoteza maisha na kupata hadhi ya shahidi ikilinganishwa na vita iliyotangulia, na pia madhara makubwa yakapatikana katika sehemu mbalimbali za nchi.

Halikadhalika amesema sasa tuko katika vita ya tatu ambavyo Katika siku yake ya kwanza, tulimsindikiza kwa macho yenye machozi na nyoyo zilizojeruhiwa baba mpendwa wa umma, Kiongozi wetu mtukufu, Mwenyezi Mungu ainue daraja lake tukufu.

Amesema vita vya sasa vilianza baada ya adui kukata tamaa ya kuona harakati kubwa ya wananchi ikiunga mkono upande wake. Kwa dhana potofu, alifikiri kwamba ikiwa ataua shahidi viongozi wa juu wa mfumo na baadhi ya watu wenye athari katika uongozi wa kijeshi, angeweza kuwatia hofu na kukata tamaa nyinyi wananchi wapendwa, na hivyo kuwafanya mjiondoe katika uwanja wa mapambano; na kwa njia hiyo kutimiza ndoto yake ya kutawala Iran na hatimaye kuigawanya vipande vipande.

Hata hivyo, katika mwezi huu mtukufu, mkiambatanisha saumu yenu na jihadi, na mkaunda mstari mpana wa ulinzi unaoenea kote nchini, pamoja na ngome madhubuti katika kila uwanja, mitaa na misikiti.

Kuhusiana na masuala ya kiuchumi, Ayatullah Mujtaba Khamenei amesema katika kufuata njia ya Kiongozi Muadhamu shahidi, ametangaza kauli mbiu ya mwaka huu  nchini Iran kuwa ni: “Uchumi wa Kimuqawama (Kimapambano) unaojengwa kwa umoja wa kitaifa na usalama wa taifa.”

Katika sehemu nyingine ya ujumbe wake, amesisitiza kuhusu umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kidugu na nchi jirani ambazo amesema zina nukta nyingi za pamoja na Iran hasa kama vile imani moja ya Kiislamu na maslahi ya pamoja katika kukabiliana na ubeberu duniani.

Pia ametoa ombi kwa ombi kwa nchi  mbili ndugu, Afghanistan na Pakistan, kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu na ili kulinda umoja wa Umma wa Kiislamu, zifanye jitihada za kuimarisha uhusiano wao. Amesema yuko tayari kuchukua hatua zinazohitajika katika mipaka ya jukumu langu.

Ayatullah Mojtaba Khamenei pia nakumbusha kwamba mashambulizi yaliyotokea nchini Uturuki na Oman, ambazo zote mbili zina mahusiano mazuri na Ira, dhidi ya baadhi ya maeneo ndani ya nchi hizo, hayakufanywa kabisa na vikosi vya kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu au na nguvu nyingine zozote za upande wa muqawama. Amesma mashambulio hayo ni njama inayotumiwa na adui wa Kizayuni kupitia mbinu ya “bendera ya uongo”, kwa lengo la kuleta mifarakano kati ya Jamhuri ya Kiislamu na majirani zake. Aidha ametayadharisha kuwa adui anaweza kukariri matukio kama hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *