Operesheni iliyofanikiwa ya makombora ya Iran dhidi ya kiwanda cha kusafisha mafuta cha Haifa imesababisha uharibifu mkubwa katika kiwanda hicho.
Kampuni ya Kusafisha Mafuta ya Haifa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) imetangaza kuwa moto katika mitambo ya kusafisha mafuta katika kiwanda hicho kufuatia shambulio la kombora la Iran umesababisha uharibifu wa shekeli milioni sita (sarafu ya utawala wa Kizayuni wa Israel).

Vile vile imeripotiwa kuwa moto uliosababishwa na shambulio la kombora la Iran bado haujazimwa.

Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Bazan huko Haifa pia kimetangaza kuwa kimepata uharibifu mkubwa baada ya shambulio la kombora la Iran.

Kwa upande mwingine gazeti la Haaretz limekiri kuwa Iran na Hizbullah ya Lebanon zimerusha makombora 1,200 kuelekea ardhi za palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *