Mkurugenzi wa zamani wa Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi cha Marekani amekiri kwamba viongozi wakuu wa utawala wa Kizayuni na washirika wake wanaochochea vita wa Marekani ndio walimshinikiza rais wa nchi hiyo kuishambulia Iran.

Joe Kent ambaye alijiuzulu wadhifa wake katika serikali ya Marekani mapema wiki hii kutokana na vita vya kichokozi vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran alisema Ijumaa kuwa viongozi wa Israel na maafisa wa Marekani walimzingira Rais Donald Trump na kuondoa pembeni yake watu wanaopinga vita na hatimaye kumshawishi aanzishe vita dhidi ya Iran.

Kent amesisitiza kuwa: Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel na washauri wake, wakisaidiwa na washirika wa Trump wanaochochea vita kama vile Seneta Lindsey Graham wa chama cha Republican, walifanikiwa kumshawishi rais huyo wa Marekani uingie vitani dhidi ya Iran kabla ya utawala wake kutathmini ipasavyo madhara yote yanayoweza kutokea.

“Juhudi zote hizi zilifanywa licha ya kukosekana ushahidi madhubuti wa tishio lililo karibu kutokea Tehran dhidi ya Marekani. Walifanya kila waliloweza kumshawishi Trump kwamba ikiwa atachukua hatua sasa, vita vitaisha haraka na kirahisi.” Amesema Kent.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi cha Marekani amekiri kwamba mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yamewaunganisha Wairani na kuwaleta karibu na mfumo unaotawala na kuwa, mauaji ya kigaidi dhidi ya viongozi wa Iran akiwemo kiongozi mkuu aliyeuawa shahidi Imam Khamenei, hayaudhoofishi mfumo wa Iran, bali yanauimarisha zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *