Waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Negamsi wilayani Babati, mkoani Manyara wamejitokeza kushiriki uchangiaji wa damu salama kwa lengo la kuokoa maisha ya wenye uhitaji.

Zoezi hilo linawalenga wagonjwa, mama wajawazito na waathirika wa ajali, likiwa sehemu ya kuhitimisha wiki ya matendo ya huruma kwa jamii.

Wakizungumza na Azam TV, baadhi ya waumini hao wamesema ni wajibu wa jamii kujitokeza kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha na kuhimiza wananchi kuachana na imani potofu kuhusu uchangiaji wa damu na kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.

✍ Hellen Kawiche
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *