Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) imezindua utafiti wa sensa ya pili ya rasilimali za uvuvi katika Ziwa Tanganyika, utakaodumu kwa siku 21 katika nchi nne za Tanzania, DRC, Burundi na Zambia.

Utafiti huo unalenga kupima hali ya wingi wa samaki na dagaa, ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango wa kufunga shughuli za uvuvi kwa miezi mitatu kila mwaka.

TAFIRI imesema matokeo ya sensa hiyo yatasaidia kutathmini mafanikio ya mpango huo na kutoa mwelekeo wa hatua zaidi za uhifadhi na usimamizi endelevu wa rasilimali za uvuvi katika Ziwa Tanganyika.

✍ Jacob Ruvilo
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *