Kinara wa Wademokrati katika Baraza la Wawakilishi la Marekani amekosoa serikali na Warepublican nchini humo kwa kuanzisha vita dhidi ya Iran na kusisitiza udharura wa kubadilishwa utawala wa Marekani.

Hakim Jafris ambaye ni mwakilishi wa New York katika Kongresi ya Marekani ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba: “Donald Trump na Warepublican wenye misimamo mikali wameanzisha vita vya kichokozi huko Magharibi mwa Asia. Sasa bei ya mafuta ya petroli imepanda kupindukia, mabilioni ya dola yanaharibiwa bure na nchi imekosa usalama zaidi. Tunahitaji kufanya mabadiliko ya utawala wa Marekani.”

Hakim Jefris ameongeza: Trump na Netanyahu wamesababisha maafa ya binadamu huko Asia Magharibi.

Wakati huo huo, Seneta wa chama cha Democratic, Elizabeth Warren amemtuhumu Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuwa wamechochea moto wa vita na kufanya maafa ya binadamu eneo la Asia Magharibi.

Elizabeth Warren

Seneta huyo wa jimbo la Masachussets amesema, Trump na Ntanyahu wameanzisha vita vya kikanda huko Asia Magharibi na kusababisha maafa ya binadamu. Hebu tazama Lebanon! Israel imeua zaidi ya raia elfu moja wa Lebanon ambao karibu asilimia 20 miongoni mwao ni watoto.

Elizabeth Warren ameongeza kuwa Kongresi haipasi kupasisha bajeti ya vita hivi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *