#HABARI: Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameshutumu Iran kwa kupanga njama za kuvuruga njia kuu za biashara duniani kwa kushambulia meli zinazopita katika Mlango-bahari wa Hormuz, ambao ni muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani.
Akizungumza akiwa kusini mwa mji wa Arad ulioshambuliwa hivi karibuni, Netanyahu amegusia kombora la Iran lililolenga kambi za kijeshi za Marekani na Uingereza katika eneo la Diego Garcia, umbali wa kilomita 4,000, kama thibitisho la kukua kwa uwezo wa kijeshi wa taifa hilo la Kiislamu.
Aidha, Netanyahu, ameionya dunia kuwa Iran imekuwa kitisho cha Kimataifa na si kwa Mashariki ya Kati pekee, akidai kuwa nchi hiyo sasa ina uwezo wa kushambulia hadi barani Ulaya.
Amesema kuwa hatua hizo za Iran zinalenga kutikisa uchumi wa dunia na usalama wa bahari, hivyo kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti kudhibiti harakati hizo kabla hazijaleta madhara makubwa zaidi katika njia hizo za kimkakati.
#DWSwahili
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)