Miaka themanini baadaye, matumaini ya amani, heshima na usawa bado yanaendelea kuhimizwa, huku Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake katika Jiji la New York mahali ambacho sasa haliwezi kutenganishwa na utambulisho wa kimataifa wa shirika hilo, lakini si kila wakati lilipangwa kuwa makazi yake.
Chuo cha Hunter ambacho sasa kinajulikana kama Lehman College kilicho katika jimbo la The Bronx, New York, kilikuwa moja ya makao ya muda ya Umoja wa Mataifa na mahali pa kikao cha kwanza cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nchini Marekani kilichofanyika 25 Machi 1946.
Mahali pekee Kikao cha Baraza la Usalama kufanyika nje ya makao yake ya Sasa
Ukumbi wa mchezo wa mpira wa chuo cha Hunter ulirekebishwa kuwa chumba cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndani ya wiki tatu tu. Waandishi wa habari walipangiwa kukaa kwenye bwawa la kuogelea lililogeuzwa kuwa ofisi. Moja ya ajenda ya kwanza iliyojadiliwa na Baraza ni Iran.
Wafanyakazi wawili wa sasa wa Chuo cha Lehman wakiwa wameshikilia picha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
kutoka 1946 ambalo liliwahi kutumia uwanja wa mpira wa vikapu wa chuo hicho kuendesha mikutano
Chuo cha Hunter haikutosha kukaa wafanyakazi wote wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wanahitajika kuendesha shirika, kwa kuzingatia pia wajumbe kutoka katika mataifa 51 wakati huo, hivyo makao mapya ya muda yaliundwa kwenye kiwanda cha silaha kilichotumika katika Vita vya Pili vya Dunia huko Lake Success, katika mji wa Long Island.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwasili Lake Success Oktoba 1946.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walifika Lake Success mwezi Oktoba 1946. Hapo, wakufunzi wa Umoja wa Mataifa walitoka katika tamaduni na asili mbalimbali duniani. Ripoti za magazeti ziligundua utofauti wa kuona wanawake wakiwa wamevaa saree na wanaume wakiwa wamevaa mavazi ya kitamaduni.
Eleanor Roosevelt (Katikati) akijumuika kwenye mjadala na UN Radio kuhusu sheria ya kimataifa ya haki za binadamu
Kwenye Lake Success, mikutano ilirekodiwa na kusambazwa duniani kote, ikiwakilisha tukio lisilowahi kutokea katika historia ya upanuzi wa matangazo ya kimataifa.
UN Radio na Azimio la Haki za Binadamu
Radio ya Umoja wa Mataifa ilianzishwa mwaka 1946 na mhojaji wa kwanza alikuwa Eleanor Roosevelt, mwakilishi wa Marekani na mwanamke aliyechochea kuundwa kwa Azimio la Haki za Binadamu. Siku ya Redio Duniani inaadhimishwa kila 13 Februari siku ambayo Radio ya Umoja wa Mataifa ilipoanza kurusha matangazo, miaka 80 iliyopita.
Kampuni ya usafirishaji ya New York ikijiandaa kuuhamisha Umoja wa Mataifa
Hali ya hewa baridi na upepo katika eneo la Flushing Meadows, jimbo la Queens, New York, ilifanya wajumbe wengi kuvaa makoti ndani ya majengo. Hali hiyo ilionesha kuwa hata diplomasia ya dunia ilikuwa ikikabili baridi ya New York. Lakini Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo Trygve Lie kutoka Norway aliita jengo na mbuga za jirani ishara yenye nguvu ya urafiki kati ya Umoja wa Mataifanna jiji lililokuwa mwenyeji.
Ukumbi wa mchezo wa kutembea kwenye barafu au skating uligeuzwa kuwa Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hadi mwaka 1950, wakati Umoja wa Mataifa ulipokuwa umepanuka hadi kuwa na Mataifa 60 Wanachama (leo una wanachama 193).
Mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa akihakiki vibao vya majina ya nchi kwa ajili ya nchi zinazoshiriki mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Flushing Meadow Queens
Wafanyakazi wa Kitengo cha Utawala cha Umoja wa Mataifa walihakikisha mikutano ya kimataifa iliyoandaliwa kwa kiwango kisichowahi kuonekana hapo awali ilikuwa inafanikiwa.
Maafisa habari wa Un wakiahikiki na kusahihisha ripoti zinazowasilishwa Barazani
Kutafuta makao ya kudumu
Jiji la New York liliwakilishwa pamoja na Boston, Philadelphia, San Francisco, na Fairfield County, Connecticut pamoja na Westchester County, New York, katika ushindani wa kupewa makao ya kudumu.
Katibu Mkuu wa Un wakati huo Trygve Lie (katikati) akipokea zawadi ya dola milioni 8.5 Machi 1947 kwa ajili ya kununua kiwanja East River in Manhattan kujenga makao makuu ya UN
Zawadi ya dola milioni 8.5 kutoka kwa mfanyabiashara maarufu John D. Rockefeller ilihakikisha kuwepo kwa eneo la ekari 17 ambalo Makao Makuuya Umoja wa Matafa yanakalia kwenye Mto wa Mashariki, mjini Manhattan. Kazi ya ujenzi ilianza mwaka 1947 na ilichukua takriban miaka mitatu, ikihusisha timu ya wabunifu mashuhuri wakiwemo Le Corbusier na Oscar Niemeyer.
Wafanyakazi walianza kuhamia jengo hilo jipya mwaka 1951, na ujenzi ulipokamilika mwaka 1952 kulikuwa na nafasi ya ofisi kwa takriban watu 3,000.
Kazi ilianza 1947 kusafisha kiwanja kwa ajili ya ujeni wa Makao Makuu ya UN
Uhusiano wa UN na New York
Uhusiano wa Umoja wa Mataifa na Jiji la New York sasa unarudi nyuma miaka 80. Mwana historia Chris McNickle anasema, “Sina shaka kuwa Umoja wa Mataifa uko mahali pale panapostahili. New York ni jiji kubwa la wahamiaji duniani. Ni ishara kwamba watu kutoka sehemu zote za dunia, rangi zote, dini zote, wanaweza kushirikiana na kuishi pamoja, na bado huu ni ukweli hadi leo.”
Wajenzi wakinawa baada ya kazi ya siku nzima kwenye makao Makuu mapya ya UN
Marekani, mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa, ilikuwa nguvu inayosukuma nyuma ya wazo na utekelezaji wa kimwili wa shirika. Balozi wa Marekani Warren R. Austin alisemawakati huo “Umoja wa Mataifa umejengwa juu ya misingi itakayodumu zaidi ya chuma na jiwe lolote. Umoja wa Mataifa unasimama, ukishikiliwa na sheria za Mungu, kama chombo muhimu zaidi cha binadamu kutatua matatizo na kuunganisha watu wa dunia.”
Msafisha Madirisha akifanya kazi yake kwenye jengo jipya la UN lililokamilika mwaka 1951
Hii ni historia ya New York kabla ya Umoja wa Mataifa kupata makao yake ya kudumu Manhattan, ikionesha jitihada za kimataifa, ushirikiano, na maono ya dunia yenye amani.