
Msemaji wa Kamandi Kuu ya Jeshi Iran ya Khatamul Anbiyaa (SAW) amesema kuiambia Marekani na Israel kwamba: Munafanya makossa kufananisha vita vyenu na taifa lenye ghera na jeshi imara la Iran na filamu za Hollywood na mashujaa za kidhahania na wa kubuni akilini, na mumeanzisha uchokozi kutokana na makosa ya kimahesabu.
Kanali wa Pili Ibrahim Dhulfiqari amesema, wanasiasa habithi na wauji wa watoto wa Kimarekani na Kizayuni wanatoa bwabwaja zao kutokea masafa ya mbali ya kanda hii na kuwafanya wanajeshi wao na raia Waislamu wa kanda hii kuwa ngao ya sera zao potofu huku wakiendelea kutoa vitisho dhidi ya Iran.
Amesema: Mnapaswa kuwajibika mbele ya wananchi wa Marekani, kwa sababu wanajeshi wa Marekani wanaendelea kuuawa kwa halaiki kila siku katika vita mlivyovianzisha kutokana na sera zenu potofu, lakini mnaficha taarifa na takwimu halisi za idadi ya wanajeshi wanauouawa na kujeruhiwa kwa taifa la Marekani na familia zao, badala yake mnachuja sana habari zinazohusiana na vita.
Msemaji wa Kamandi Kuu ya Jeshi la Iran amesema: Iwapo jeshi la watendajinai litatangaza takwimu halisi za wanajeshi waliouawa na kujeruhiwa kwa wakati, mbali na suala hilo kusambaratisha jeshi lioga na kuanzisha uasi wa wanajeshi dhidi ya makanda wao, basi mtakabiliana na hasira kubwa na upinzani wa wananchi wenu wenyewe huko Marekani ambao hawatawaruhusu kuwatuma watoto wao katika meno ya mauti.
Kanali Dhulfiqari amesema: Enyi wanasiasa, hasa Donald Trump, Rais wa Marekani! Hamuwezi kupata lolote kwa vita na uchokozi wenu dhidi ya Iran kwa sarakasi ya vyombo vya habari.
Kanali Dhulfiqari ameendelea kuwaambia wanasiasa wa Marekani kwamba: Mumelidhalilisha jeshi na silaha zenu za kisasa katika vita mlivyoanzisha dhidi ya Taifa la Iran na kudunisha nara zenu za uongo katika fikra za walimwengu; huu ni ushindi mkubwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na taifa lake shujaa ambalo liko mstari wa mbele wa Umma wa Kiislamu kote duniani katika kupambana na hulka ya uvamizi na ubabe wenu. Tunaendeleza njia hii hadi tutakapofika kwenye kilele cha ushindi.
Msemaji wa Kandi Kuu ya Khatamul Anbiyaa amesema: Mmefanya makosa kufananisha vita na taifa shupavu la Iran na jeshi lake imara na filamu za Hollywood na mashujaa wake za kubuni akili. “na hapana nusra ila itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwenye Hikima”.