Nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ya soka (Taifa Stars), Simon Msuva, ameshindwa kujiunga na kambi ya timu hiyo kufuatia hali ya taharuki ya kiusalama inayotokana na mvutano wa kivita kati ya Iran na Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi, amesema kuwa Msuva amekosa usafiri wa ndege wa kutoka nchini Iraq anakocheza soka la kulipwa, hali iliyosababisha kubaki huko na hivyo kukosa michuano ya FIFA Series itakayofanyika nchini Rwanda mwishoni mwa mwezi huu.

Msuva, ambaye anakipiga katika Klabu ya Al Talaba tangu mwaka 2024, amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Taifa Stars na hujumuishwa mara kwa mara katika kikosi hicho.

Hata hivyo, safari hii hatakuwepo kutokana na changamoto ya usafiri iliyosababishwa na hali ya usalama katika eneo hilo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *