
Sauti za kupinga sera za vita za Rais Donald Trump zinaendelea kuongezeka nchini Marekani huku wananchi na familia za wanajeshi wanaotumwa Mashariki ya kati kwa ajili ya vita vya nchi hiyo na Irael dhidi ya Iran zikisema watoto wao wanauawa kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Ni baada ya Wanajeshi wa Marekani kusema kuwa hawako tayari kuendelea kuuawa kwa sababu ya kulinda maslahi ya Israel katika vita vya sasa dhidi ya Iran.
Mtandao wa habari wa al Mayadeen umeripoti kuwa, tovuti ya Kimarekani ya Haffington Post imeashiria hatua ya wanajeshi wa Marekani wanaokataa kwenda kupigana vita na Iran kwa manufaa ya Israel na kuwanukuu wakisema: Kamwe hatutapigana vita kwa sababu ya Israel.
Wakati huo huo, Seneta Mark Warner wa Marekani amesema kuwa, uhai wa wanajeshi wa Marekani unawekwa hatarini katika vita vilivyoanzishwa na Donald Trump.
Warner ameongeza kuwa, familia za wanajeshi wa Marekani zinayo haki ya kutaka maelezo ya wazi kutoka kwa makamanda wao juu ya malengo ya vita vya sasa dhidi ya Iran.
Awali, Msemaji wa Kamandi Kuu ya Jeshi Iran ya Khatamul Anbiyaa (SAW) alikuwa amesema kuiambia Marekani na Israel kwamba: Munafanya makosa kufananisha vita vyenu na taifa lenye ghera na jeshi imara la Iran na filamu za Hollywood na mashujaa za kidhahania na wa kubuni akilini, na mumeanzisha uchokozi kutokana na makosa ya kimahesabu.
Kanali Ibrahim Dhulfiqari amesema: Mnapaswa kuwajibika mbele ya wananchi kwa sababu wanajeshi wa Marekani wanaendelea kuuawa kwa halaiki kila siku katika vita mlivyovianzisha kutokana na sera zenu potofu, lakini mnaficha taarifa na takwimu halisi za idadi ya wanajeshi wanauouawa na kujeruhiwa kwa taifa la Marekani na familia zao, badala yake mnachuja sana habari zinazohusiana na vita.