Wakati dunia inaadhimi­sha Siku ya Maji Duniani chini ya kaulimbiu “Maji na Jinsia,” bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji unaothiri kwa kiasi kikubwa wanawake na wasi­chana na hilo limeonekana katika maeneo mengi ya Afrika Mashariki, hususan Tanzania vijijini.

Wanawake na wasichana hulazimika kutembea umba­li mrefu kutafuta maji, mara nyingi kabla ya mapambazu­ko au baada ya jua kuzama.

Kwa kufanya hivyo, huji­kuta wanalazimika kukosa masomo, kushindwa kush­iriki katika shughuli za kiu­chumi, na wakati mwingine hujiweka katika hatari ya kiafya na kiusalama.

Hivyo basi, upatikanaji wa maji si suala la uhai pekee, ni suala la usawa, fursa, usal­ama na utu wa binadamu. Mifumo ya maji inaposhind­wa kufanya kazi, muda wa wanawake hupotea, elimu ya wasichana huathirika, na ustawi wa familia hudorora.

Lakini mifumo ya maji inapofanikiwa, wanawake hupata muda wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi, uongozi na maendeleo ya jamii. Miundombinu ya maji inayozingatia jinsia ni hitaji la msingi la maendeleo.

Wanawake na upatikanaji wa maji

Nchini Tanzania, Water­force Africa Ltd inaonyesha namna uhandisi wa maji unavyoweza kukabili chan­gamoto hizi kwa makusudi.

Kampuni hii inayoongoz­wa na wazawa inaona upati­kanaji wa maji si suala miun­dombinu tu, bali ni uwajibi­kaji wa kijamii, ujumuishi na uwezeshaji wa jamii.

Kwa kuzingatia uende­levu, matumizi ya wazawa kwenye miradi ya maji na mifumo jumuishi inayotam­bua jinsia, kampuni hii ina­leta mageuzi namna jamii, taasisi na viwanda vinavy­opata na kusimamia maji.

“Tukibuni mifumo ya maji na usafi wa maz­ingira, tunajiuliza swali rahisi tu! Nani anafai­dika zaidi?” anasema Mkurugenzi Mtendaji wa Waterforce Africa Ltd, Shivanand Poojari.

“Ninaamini ukimweze­sha mwanamke, umeiinua jamii nzima. Wanawake wanapowezeshwa kwenye eneo la usimamizi na upati­kanaji wa maji, jamii nzima inanufaika kwa kuwa na afya, elimu na uzalishaji bora,” anasema Mkurugenzi huyo.

Kampuni imekuwa ikiz­ingatia makundi ya aina yote, ikiendelea kukuza ujumuishi miongoni mwa wafanyakazi wao na usimamizi wa miradi mbalimbali, anaeleza Mku­rugenzi.

Miradi ya Waterforce Africa Ltd imejengwa juu ya uhalisia wa mahitaji ya jamii. Visima virefu, pampu za maji zinazotumia nishati ya jua, matenki ya kuhifadhia maji na mitandao ya usambazaji hutengenezwa kimkakati karibu na makazi, shule na vituo vya afya ili kupunguza umbali wa kutafuta maji, anafafanua.

Vilevile, kulingana na Mkurugenzi huyo, miun­dombinu ya usafi wa maz­ingira imeundwa kwa kuz­ingatia faragha na heshima, hususan kwa wasichana balehe.

Hatua hizi hupunguza adha za kila siku za kuta­futa maji, huboresha usafi na afya, na kuwapa muda zaidi kwa ajili ya masomo, biasha­ra ndogondogo na malezi ya familia, anaongeza.

Zaidi ya miundombinu, anasema Waterforce Africa Ltd huziwezesha jamii kusi­mamia mifumo yao ya maji. Ushiriki wa wanawake katika kamati za maji huhamasish­wa, na wanajamii hupatiwa mafunzo ya uendeshaji na matengenezo ya msingi.

“Wanawake wana­poshirikishwa katika maamuzi, mifumo hufanya kazi vizuri zaidi, jamii hus­tawi, na wasichana hubaki shuleni,” anaeleza Mkuru­genzi Mtendaji.

Mtambo wa kutibu maji wenye uwezo wa kutibu lita 10,000 kwa saa, unaotumia teknolojia ya hali ya juu ya kuchuja maji (Nano Filtration), uliofungwa katika kampuni ya Irvine’s jijini Arusha.

Usambazaji maji kwenye viwanda na taasisi

Mbali na kuziwezesha kaya maskini kupata maji safi, anasema WaterForce imejipambanua katika kui­marisha sekta ya viwanda na taasisi nchini.

Kwenye Kiwanda cha Mtibwa Sugar Limited, kampuni ilibuni na kusanifu mfumo jumuishi wa kutibu maji wenye kifaa cha kusafi­sha maji (clarifier) chenye uwezo wa mita za ujazo 150 kwa saa, mfumo wa uchujaji maji (ultrafiltration) wa mita za ujazo 40 kwa saa, pamoja na mtambo wa usafishaji wa maji (Reverse Osmosis) wa mita za ujazo 30 kwa saa.

Mfumo huu ulidhibiti changamoto ya tope nyingi (turbidity) na kukidhi viwan­go vya juu vya uchemshaji maji, na hivyo kuboresha ufanisi wa utoaji mvuke, ubora wa kiutendaji na uza­lishaji wa kiwandani kwa ujumla.

Pale Zanzibar, mtambo wa usafishaji maji (Reverse Osmosis) wenye uwezo wa mita za ujazo 20 kwa saa ulio­fungwa katika Kiwanda cha Ikraam Bottlers and Cream­ery Limited unahakikisha upatikanaji wa maji salama ya kunywa kwa matumizi ya umma na kusaidia sekta ya utalii, anabainisha Poojari.

Aidha, anasema Kule Kwa­la Industrial Park, Eneo la Hifadhi ya Viwanda la Sino–Tanzania, WaterForce Afri­ca Ltd inaendelea na ufun­gaji wa mtambo wa kutibu majitaka wenye uwezo wa KLD 500, kuhakikisha usi­mamizi bora wa maji taka katika eneo hilo la viwanda, usafirishaji na biashara lin­alokua kwa kasi zaidi.

Anasema kuwa hatua hiyo inadhihirisha umuhimu wa kujumuisha miundombinu ya mazingira katika mipan­go ya ukuzaji wa sekta ya viwanda nchini.

Kujenga uhimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Mabadiliko ya tabianchi yanakwamisha dhamira ya dhati iliyonayo WaterForce kuwa uhalisia. Ukame, mvua zisizotabirika na changamo­to za umeme vinatishia usal­ama wa maji Afrika Mashari­ki, anasema na kuongeza.

Hivyo, hivi sasa masu­luhisho ya kampuni yame­buniwa kwa kuzingatia uimara na hii ni pamoja na uendelezaji wa maji ya chini ya ardhi kwa tafiti za kitaal­amu za kijiolojia, matumizi ya pampu za nishati ya jua, teknolojia za urudishaji maji katika matumizi mapya na uchakati maji upya, pamo­ja na mifumo ya matibabu inayoweza kushughulikia ubora tofauti wa maji.

“Uhimilivu unamaanisha miundombinu inayofanya kazi hata katika miezi mika­vu zaidi au wakati umeme unapokatika,” anasema Poojari. “Jamii na viwanda vinahitaji maji ya uhakika bila kujali hali ya hewa.”

Ahadi ya uendelevu na matumizi ya wazawa

Waterforce Africa Ltd, kulingana na Poojari, inaji­tofautisha kwa kutumia vip­aji vinavyopatikana nchini, uwezo wa uzalishaji vifaa vyake yenyewe, utaalamu wa kihandisi, na uendelevu wa muda mrefu wa miradi ya maji.

Miradi haitekelezwi tu na kuachwa; huanzishwa rasmi, hufuatiliwa na kutun­zwa. Waendeshaji wazawa hufundishwa namna sahihi ya kuisimamia ili kuhakiki­sha mifumo inaendelea kutoa huduma kwa muda mrefu baada ya kukamilika, anaeleza.

Ushirikiano na taasisi za serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, waendelezaji wa viwanda na washirika wa kimataifa wa teknolo­jia ni chachu ya mafanikio ya miradi ya kampuni hiyo, hatua inayohakikisha inaba­kia kuwa imara kiufundi, ina thamani sawa ya fedha ya uwekezaji wake na jumuishi kwa jamii yote.

“Usalama wa maji ni usalama wa taifa,” anaonge­za Mkurugenzi Mtendaji. “Tanzania ina vipaji vingi, teknolojia na uwezo wa sekta binafsi wa kutatua changa­moto za maji, kinachohitaji­ka ni ushirikiano na dhamira ya pamoja.”

Athari halisi, mabadiliko ya kudumu

Matokeo yanaonekana wazi. Jamii zilizokuwa ziki­tumia muda mwingi kuta­futa maji sasa zinapata maji salama na ya uhakika karibu na makazi yao. Mahudhurio shuleni yanaongezeka, husu­san kwa wasichana.

Wanawake sasa wanapa­ta muda wa kushiriki kati­ka shughuli za kiuchumi na uongozi. Afya za jamii zinaimarika, na viwanda vin­afanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kuharibu mazingira.

Katika Siku hii ya Maji Duniani, simulizi ya Water­force Africa Ltd inaonesha uhusiano wa kina kati ya upatikanaji wa maji, usawa wa kijinsia na maendeleo ya kiuchumi.

Ikiwa kama mzalishaji halisi wa vifaa, kampuni hiyo inaamini kuwa Tanzania laz­ima iendelee kujenga uwezo wake wenyewe wa uhandisi wa miundombinu ya maji.

Lakini miundombinu pekee haitoshi, mifumo laz­ima iwe jumuishi, imara na isimamiwe kwa uendelevu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *