Imeelezwa mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea hapa nchini yamekua yakimsababishai mkulima kupata hasara ya mazao hivyo kushauriwa kutumia kilimo cha ikolojia kuweza kusaidia kupambana na hasara hizo zinazomfikia mkulima.
Ni ziara ya waandishi wa habari za kilimo wakiwa mkoani arusha kwa uratibu wa shirika lisilo la kiserikali la island of peace wameweza kuwatembelea wakulima mbalimbali ambapo wakulima hao wamedai mabadiliko ya tabia nchi yamesababisha kupata hasara kwenye kilimo hivyo kilimo cha ikolojia kimeweza kusaidia mkulima kupata faida.
Akiongea na waandishi wa habari juu ya mafanikio kwa wakulima wanaotumia kilimo ikolojia kupitia mradi wa kilimo endelevu msimamizi wa miradi kutoka shirika la island of peace Linda Temba amesema wameweza kuwafikia wakulima 1,500 kupitia vikundi 42 kwenye vijiji 20.
Naye mkuu wa idara ya kilimo,mifugo na uvuvi halmashauri ya wilaya ya arusha Rorbart Urasa amesema serikali imendelea kuwasaidia wakulima ambao wanatumia kilimo ikolojia waweze kuzalisha kwa tija.
Aidha meneja wa miradi wa shirika la RECODA Dr Silvesta masanja amesema kilimo ikologia kinaweza kusaidia kupunguza changamoto ya rutuba kwenye ardhi.
(Feed generated with FetchRSS)