Timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars imepoteza mchezo wa kirafiki maarufu kama FIFA Series kwa bao 1-0 dhidi ya Liechtenstein kutoka Ulaya.
Katika mchezo huo ambao umechezwa Uwanja wa Pele, Rwanda Taifa Stars imeshindwa kutumia nafasi ambazo imetengenezwa na kuhukumiwa kwa kosa hilo moja na mechi kumalizika kwa Tanzania kupoteza.
Leichtenstein nchi yenye jumla ya watu Elfu 40 nchi nzima inaibuka kidedea baada ya kucheza mechi 13 bila ushindi.
Taifa hilo ambalo liko katikati ya Austria na Uswizi kwenye viwango vya ubora wa FIFA inashika nafasi ya 205 kati ya timu 211 huku Tanzania ikishika nafasi ya 110.
Ikumbukwe Taifa Stars chini ya Miguel Gamondi mpaka leo haijui ladha ya ushindi kwani ni vipigo na sare.

(Feed generated with FetchRSS)