Kampuni ya vinywaji baridi ya Azam Soda and Juice imetambulisha kinywaji kipya cha MOJITO SODA chenye ladha ya limao na mint, ambacho kimepokelewa vyema na wananchi waliotembelea maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Kinywaji hicho kimezua mvuto mkubwa katika maonesho ya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, huku wananchi wengi wakionesha kuvutiwa na ladha yake mpya na ubunifu wake. Kwa mujibu wa Joseph Mpangala, bidhaa hiyo mpya inaendelea kupata mwitikio chanya kutoka kwa watumiaji waliotembelea banda la kampuni hiyo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)