Asubuhi ya Jumamosi, Februari 28, 2026, Israel na Marekani zilianza rasmi kuishambulia Iran kwa pamoja ambapo mwanzoni kabisa mwa shambulio hilo, zilimuua shahidi Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mauaji hayo ya kigaidi yalitekelezwa huku mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Iran na Marekani yakiendelea.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, akiwa na matumaini makubwa aliripoti kuwepo kwa maendeleo ya kutia moyo katika mazungumzo hayo kwa viongozi wakuu wa Marekani. Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki alikuwepo kwenye mazungumzo ya Geneva kama mwangalizi na mshiriki. Rais Trump mwenyewe alikuwa ametangaza kwamba kikao cha baadaye kingefanyika Ijumaa iliyofuata. Hata hivyo, Netanyahu mbaguzi wa rangi alikuwa ametangaza mapema kwamba angefanya kila aliloweza kuhujumu na kuvuruga mazungumzo hayo. Hii ilikuwa mara ya pili kwa Trump kutoa mhanga na kuhatarisha usalama wa dunia kwa ajili ya kuhudumia matakwa, tamaa na chokochoko za Netanyahu mtenda-jinai. Ukweli ni kwamba wahalifu wawili hawa wenye nia mbaya wamefanya siasa na diplomasia kutofanya kazi tena duniani. Kama wanavyofanya matapeli, hutoa matamshi kila mara na kisha kutenda kinyume chake, na hivyo kuwasha moto katika pembe tofauti za dunia.

Matarajio ya Iran kutoka kwa majirani zake wa nchi za kusini mwa Ghuba ya Uajemi ni kwamba kwa uchahce wangetuma salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Iran kwa mnasa wa kuuawa kigaidi kiongozi mkuu wa Iran na kulaani mashambulizi ya kichokozi ya Israel na Marekani, mashambulizi ambayo yalifanywa bila sababu yoyote halali na bila kupitia mchakato wowote wa kisheria katika Umoja wa Mataifa. Isitoshe, si tu kwamba walikataa kutuma salamu zozote za rambirambi, bali pia walidai kuwa wana haki ya kulipiza kisasi dhidi ya Iran baada ya Iran kuamua kulipisa kisasi cha mashambulio yaliyofanywa na Marekani kutokea kwenye vituo vyake vya kijeshi vilivyoko katika ardhi za nchi za Kiarabu. Nchi hizo hizo zilifanya makosa kama hayo wakati wa uchokozi wa Saddam wa Iraq dhidi ya Iran.

Hata hivyo mara hii ilitarajiwa kwamba nchi hizo zingesimama na jirani yao mwenye subira kubwa na Mwislamu Iran, ambaye alishambuliwa na utawala wa kibaguzi wa Kizayuni ukishirikiana na mwingine wa kikafiri wa Marekani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Aidha Iran ilikuwa tayari imewaonya kwamba, kama ingeshambuliwa na Israel na Marekani kutokea kwenye ardhi zao, vita vingekuwa vya kieneo. Je, wanawezaje kukaa kimya mbele ya uchokozi wa mtenda-jinai Netanyahu—ambaye anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kwa tuhuma za mauaji ya halaiki na ambaye amewaua bila huruma Waarabu Wapalestina zaidi ya 70,000—na kisha kusimama na wachokozi dhidi ya Iran?

Trump na Netanyahu, wahalifu na magaidi wakubwa duniani

Lingekuwa jambo la busara kama majirani hawa wa Iran wa kusini mwa Ghuba ya Uajemi kwa uchache wangezingatia msimamo wa Uingereza. Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyobuni Israel na mshirika wa kistratijia wa Marekani, hakukubali kamwe kuviita vitendo vya wahalifu hawa wawili wa kimataifa kuwa ni halali. Hata kama aliwasaidia kimya kimya baadaye lakini alijiepusha kuhalalisha hatua zao hizo za kijinai na kigaidi. Pamoja na hayo, lakini Iran yenye subira na moyo wa kusamehe inawaambia kuwa hawajachelewa sana, bado wanayo fursa ya kujirudi na kurekebisha makosa waliyofanya. Ingekuwa vyema kwao, badala ya kujiweka katika kambi inayoongozwa na mhalifu Netanyahu, wasimame pamoja na Iran na kutafuta njia za kujidhaminia usalama wao wenyewe badala ya kuwategemea wageni wasiowajali na ambao wanatufata tu njia za kupora mali na utajiri wao kwa madhara ya Uislamu na Waislamu. Wanapasa kushirikiana na Iran, Pakistan na China katika kubuni na kuanzisha mfumo wa usalama wa kikanda kwa ajili ya kulinda kwa pamoja minyororo ya usambazaji wa nishati na thamani za bidhaa kimataifa. Ni wazi kuwa, kualikwa Umoja wa Ulaya na Marekani kujiunga na mifumo ya usalama wa eneo katika hatua za baadaye si tatizo. Tuna wajibu wa kudhamini usalama wa kikanda na kimataifa kwa ajili ya wote.

Hivi karibuni au baadaye, mzozo huu utaisha, ambapo Marekani itaondoka katika eneo hili, lakini kijiografia, nchi za eneo zitalazimika kuendelea kuishi pamoja kama majirani. Siku chache tu zilizopita, Balozi wa Marekani katika utawala wa Israel alikubaliana na fikra ya utawala huo ya kunyakua ardhi zote za nchi za Kiarabu zilizoko kati ya Mto Nile na Euphrates. Bila shaka, Israel, kama uvimbe mkubwa wa saratani, ndio chanzo kikuu cha tishio kwa nchi zote za eneo la Mashariki ya Kati.

Katika wiki chache zilizopita, nchi za eneo hili zimeona waziwazi kwamba Marekani na Israel hata hazina uwezo wa kulinda maslahi na vituo vyao zenyewe katika eneo, achilia mbali kuwajibika kuwalindia wengine usalama wao. Kwa hivyo, lingekuwa jambo la busara kama nchi zote za eneo zingeamua kushirikiana kwa pamoja katika kutafuta njia za kujidhaminia usalama wao zenyewe, badala ya kuchochewa na wageni zipigane na kugombana mara kwa mara kwa maslahi ya watenda jinai za kivita na wauaji wa watoto wadogo Netanyahu na Trump, wanaokodolea macho mafuta na utajiri wao bila kuchoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *