
Baraza la tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, limepitisha azimio linaloagiza uchunguzi wa haraka kuhusu madai ya vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na uhalifu wa kivita vilivyotekelezwa kuzunguka mji wa El Obeid nchini Sudan, mji ambao umezingirwa na wapiganaji wa RSF.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uingereza ambayo ndio iliwasilisha azimio hilo pamoja na mataifa mengine 14, ilikuwa imeonya kuhusu kutokea kwa ukiukaji wa haki za binadamu baada ya RSF kuongeza idadi ya wapiaganaji wake kwenye Mji huo.
Wiki iliopita, Baraza hilo kwenye ripoti yake, lilithibitisha kurekodi visa vingi vya ukiukaji wa haki za binadamu katika Mji wa al-Obeid, ikiwemo kunyongwa kwa raia, utekaji wa watu, utesaji pamoja na ukatili wa kijinisia miongoni mwa vitendo vingine.
RSF imekuwa ikikanusha kuhusika na ukandamizaji wa haki za binadamu katika vita vyake vya zaidi ya miaka mitatu na jeshi la serikali ya Sudan, ikidai kuwa ripoti hizo zimechochewa na maadui wake.
Haya yanajiri wakati huu mkuu wa masuala ya misaada ya kibinadamu wa umoja wa Mataifa, akithibitisha kuzungumza kwa simu na mkuu wa RSF jenerali Muhammad Hamdani Dagalo, maarufu kama Hemedti.