Wakuliama wa parachichi wa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameipongeza serikali kwa hatua za kudhibiti uholelela katika biashara ya zao la parachichi.
Frank Mwankenja ambaye ni mkulima wa parachichi amesema hatua za kuwatambua na kuwasajili wanunuzi na mawakala wa zao la parachichi imesaidia kutatua changamoto changamoto nyingi ikiwemo wizi wa matutanda mashambani na utapeli uliokuwa ukifanywa na baadhi ya madalali wasio waaminifu.
Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA),inaendelea na urasimishaji wa biashara ya zao la parachichi kwa kuwasajili wanunuzi na mawala kwa lengo la kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara.
(Feed generated with FetchRSS)