Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaonya Wamarekani akisema: “Mara tu manowari ya kubeba ndege ya Abraham Lincoln itakapokaribia eneo letu la ulengaji shabaha, tutalipiza kisasi cha damu ya mashahidi wa manowari ya Dena kwa kurusha aina mbalimbali ya makombora kutoka pwani hadi baharini.”

Admeri Shahram Irani, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amewaambia askari wa vitengo vya makombora, ndege zisizo na rubani na ulinzi wa anga za jeshi hilo kwamba: “Awali, na kupitia hatua kadhaa za operesheni za makombora za Jeshi la Wanamaji dhidi ya manowari ya Abraham Lincoln, meli hii na nyingine ya kivita zililengwa, na wahalifu hawa wa Kimarekani wakaingiwa na hofu kubwa ya kushambuliwa na makombora yetu ambapo walilazimika kuhamahama na kuihamishia manowari hii umbali wa mamia ya maili kutoka maji ya Iran.”

Ameongeza: “Ikiwa meli hii itaingia ndani ya eneo la shabaha ya makombora yetu, tutalipiza kisasi kwa kurusha aina mbalimbali za makombora ya kutoka pwani hadi bahari katika pwani ya Makran.”

Huku akiashiria kimya cha CENTCOM kuhusu mashambulizi na uharibifu uliofanywa na majeshi ya Iran dhidi ya vitengo vya wanamaji wa Marekani vilivyopo katika eneo, Admeri Irani amesema: “Maeneo yote ya harakati za manowari ya Abraham Lincoln na maombi yake kwa nchi za eneo kwa ajili ya kupewa huduma na mahitaji mengine ya msaada, yanafuatiliwa kwa karibu na kwa umakini na vikosi vya Iran.”

Amesema: “Mashariki mwa Lango-Bahari la Hormuz na Bahari ya Oman, ambao unachukuliwa kuwa mwanzo wa kuingia katika Lango-Bahari la Hormuz na Ghuba ya Uajemi, uko chini ya udhibiti kamili wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na tunasubiria wakati wa kulipiza kisasi dhidi yenu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *