Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la ndizi la Mula, lililopo Kata ya Masama Mashariki, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa soko jipya ili kuondokana na changamoto ya miundombinu duni katika eneo la kuuzia bidhaa hiyo ambalo huzingirwa na maji na matope wakati huu wa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini.

Wafanyabiashara hao wamesema wanakumbana na ugumu katika uendeshaji wa biashara zao kutokana na hali ya soko hilo kujaa matope, na hivyo kuhatarisha usalama wa chakula na hivyo kupunguza idadi ya wateja Sokoni hapo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *