
DAR ES SALAAM: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amesema uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya Dough Works Ltd umesaidia kuiunga mkono serikali kwa kuwapa vijana ajira zaidi ya 800 jambo ambalo limesaidia kukua kwa uchumi katika wilaya hiyo.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mgahawa wake katika eneo la Kunduchi Mall nakusema kuwa serikali peke yake haitaweza kuajiri kila mtu hivyo sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kuchechemua uchumi.

“Tunafurahia uwekezaji huu na tunafahamu mheshimiwa Rais wetu aliamuru kwamba tuunganishe nguvu tuipiganie nchi yetu na ameenddlea kuiunganisha nguvu na ametoa makuwa tunafahamu serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu hivyo uwekekezaji huu ni mkubwa katika wilaya yetu,”amesema Mtambule.
Kwa Upande wake Viloleth Temba Meneja Rasilimaliwatu Kampuni ya Dough Works Ltd amesema ni ufunguzi wa mgahawa wa 13 wa KFC na wa 9 Pizza Hut nchini na umewaajiri wananchi zaidi ya 800 katika maeneo yote migahawa hiyo ilipo