
Jeshi la mapinduzi la Iran (IRGC) limethibitisha rasmi kuuawa kwa Alireza Tangsiri, kamanda wa jeshi lake la maji siku nne kupita tangu jeshi la Israeli kutangaza kumuuwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na taarifa ya IRGC, Tangsiri alikuwa akilinda maeneo ya pwani ya Iran pamoja na vikosi vyake na alifariki kutokana na majeraha mabaya.
Licha ya kuuawa kwake, wanajeshi wa maji wamesema wataendelea na majukumu yao kama kawaida ikiwemo kulinda mlango wa bahari wa Hormuz.
IRGC imeapa kuendelea kupigana hadi kile imekitaja kama adui kuharibiwa kabisa.
Tangsiri, mmoja wa makanda wa ngazi ya juu wa jeshi la IRGC alikuwa na majukumu ya kusimamia namna mali za mafuta zinapita katika mlango wa Hormuz.
Kulingana na taarifa yake kwenye mtandao wake wa X kabla ya kifo chake, Tangsiri alikuwa ameapa kwamba hakuna meli ya adui itakayoruhusiwa kupita kwenye mlango wa Hormuz.
Mwaka wa 2019, Tangsiri alitangaziwa vikwazo na Wizara ya fedha ya Marekani baada ya Iran kuangusha ndege ya kijasusi ya Washington kwenye mlango wa Hormuz.