Katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania, Wakulima wa Mkoa wa Dodoma wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake katika uasisi wa Programu ya Jenga Kesho iliyobora maarufu kama (Building Better Tomorrow- BBT), wakisema kupitia programu hiyo wameendelea kunufaika zaidi na kilimo pamoja na kuondokana na umaskini wa kipato licha ya ukame unaoshuhudiwa katika Mkoa huo wa Katikati mwa nchi.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Machi 29, 2026, wakulima hao ambao ni wanufaika wa programu hiyo ya BBT kutoka kwenye kikundi cha wakulima wadogo cga Wanyeusi kinachopatikana Kijiji cha Manchali A, Wilayani Chamwino, wamesema kupitia maono ya Rais Samia wameondokana na kilimo cha msimu mmoja kwa mwaka hadi kuwa na Kilimo cha mara nne kwa mwaka, suala ambalo limefungua kurasa mpya ya kilimo cha kisasa, chenye tija na uhakika wa mavuno.

#kilichoborakabisa

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *