“Hakuna anayepaswa kupoteza maisha akihudumia amani,” umesema ujumbe wa UNIFIL ukisisitiza haja ya kulindwa kwa walinda amani na raia wanaowahudumia.

Askari huyo, raia wa Indonesia, aliuawa jana Jumapili akiwa ndani ya kituo cha UNIFIL huko Ett-Taibe wakati wa mapigano yanayoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah wanaopinga mashambulizi dhidi ya Iran.

Mwanamke aliyehamishwa akiwa amevaa hijab na kumshika mtoto mchanga ameketi kando ya rundo kubwa la masanduku ya misaada ya chakula ya UNICEF na WFP nchini Lebanon.

© WFP/Marco Frattini

Usambazaji wa Msaada wa kibinadamu kwa familia za wakimbizi kaskazini mwa Lebanon.

Raia na wahudumu wa mstari wa mbele washambuliwa

Ghasia hizo pia zimeathiri vibaya raia. Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, iesema imeshtushwa na taarifa za kuuawa kwa wahudumu 9 wa afya na wanahabari 3 katika mashambulizi ya anga ya Israel nchini Lebanon.

Imesisitiza kuwa wahudumu wa afya na waandishi wa habari wanalindwa chini ya sheria za kimataifa na hawapaswi kushambuliwa.

Juhudi za kidiplomasia kuimarisha njia muhimu

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umeanzisha kikosi kazi kipya kurejesha usafirishaji wa mbolea na misaada ya kibinadamu kupitia Mlango wa Bahari wa Hormuz.

Hatua hiyo inakuja huku usumbufu wa usafirishaji ukitishia minyororo ya ugavi duniani, na maafisa wa Umoja wa Mataifa wakionya athari za kiuchumi zinaweza kuenea kimataifa.

Jua linapochomoza nyuma ya moshi mkubwa wa viwanda unaoinuka juu ya eneo la jiji la Tehran nchini Iran.

Domain ya Umma

Tehran, Iranmoshi ukitanda angani kufuatia mashambulizi ya Israel na Marekani

Kituo cha Iran chashambuliwa huku wasiwasi wa nyuklia ukiongezeka

Kuhusu usalama wa nyuklia katika vita hivyo Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomic IAEA limethibitisha kuwa kituo cha uzalishaji wa maji mazito cha Khondab nchini Iran kimeharibiwa vibaya kufuatia shambulio la tarehe 27 Machi.

Ingawa limesema hakuna mionzi ya nyuklia iliyoripotiwa kuwepo, kituo hicho sasa hakifanyi kazi, hali inayoongeza wasiwasi kuhusu usalama wa miundombinu ya nyuklia.

Hofu ya vita vya kikanda yaongezeka

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa hofu inaongezeka ya mgogoro huo kusambaa kzaidi kikanda.

Kwani mvutano pia unaongezeka Yemen, ambapo Hans Grundberg mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Yemen  ameonya kuwa hatua ya Wahouthi kujiunga na vita dhidi ya Israel inaweza kuingiza nchi hiyo zaidi katika mgogoro.

“Hatua hii ya kuongeza mapigano inaweza kuifanya Yemen iingie katika vita vya kikanda na kuongeza mateso ya raia,” amesema, akisisitiza kuwa hakuna upande unaopaswa kupanua wigo wa vita kwa upande mmoja.

Dina, mfanyakazi wa misaada wa Palestina, anasimama na wenzake wawili wakati wanapobeba mifuko mikubwa ya misaada ya kibinadamu kwenye ghala katika Jiji la Gaza. Kikundi hicho kinafanya kazi chini ya hali ngumu ili kutoa misaada muhimu ya chakula kwa watu wenye uhitaji.

© WFP/Maxime Le Lijour

Msaada wa chakula unatayarishwa ili unawafikia watu katika eneo lote la Gaza.

Mgogoro wa kibinadamu unashika kasi

Katika Ukanda wa Gaza, nako uharibifu ni mkubwa, huku nyumba, barabara na miundombinu muhimu vikiharibiwa, na jamii nyingi kubaki bila makazi katika hali ngumu.

Kamishina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Philippe Lazzarini ameelezea hali hiyo kama “janga la kibinadamu,” wakati Umoja wa Mataifa ukionya kuwa athari zinaenea zaidi ya kanda hiyo.

Mashirika ya kibinadamu nayo yanaonya kuwa hadi watu milioni 17 zaidi barani Afrika wanaweza kukumbwa na njaa kali kutokana na kuporomoka kwa minyororo ya ugavi na kupanda kwa bei za chakula. Zinazotokana na changamoto katika mlango bahari wa Hormuz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *