Nchini DRC, raia bado wanaendelea kusherehekea ushindi wa timu yao ya Léopards iliyofuzu kushiriki mashindano ya kombe la dunia kufuatia ushindi wao wa 1- 0 dhidi ya Jamaica. Mjini Bukavu wakazi pia wamesherehekea.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Akiwa amevalia jezi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku akisakata muziki wa Fimbu, Julien M14 ni mmiliki wa duka ndogo linalouza jezi za timu ya taifa.

”Tangu nizaliwe, sijawahi kuona timu yangu ikifuzu kwa kombe la dunia. Ninafuraha sana. Jezi nauza hapa, watu wananunua haraka”

Nelly Amani, shabiki mwingine wa Léopards naye pia ni mwenye furaha tele.

“Timu yetu ya Leopards imetuondolea aibu, ndiyo maana nimevaa jezi hii ya DRC. Nilibaki nyumbani, lakini kama ningekuwa na pesa ningeweza kwenda kusherehekea ushindi huu, kwa bahati mbaya, sikuwa na pesa ndio sababu sikwenda.”

Licha ya sherehe hizo mjini Bukavu, baadhi ya watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Pacifique Bahumeokunanwa ni mmoja wao.

“Tulienda kutafuta. Ikiwa hutatoka nyumbani familia zetu zitaishi vipi? Hatupati chochote tena. Hatukuwa na chaguo ila kuona jinsi familia zetu zingepata chakula. Lakini tuna furaha kabisa”.

François Bayubasire kwa upande wake amekuwa na kauli hili.

”Tuliweka dau la pesa zetu kwenye kamari, lakini zimepotea. Ni kweli tulishinda, lakini ilikuwa mechi ngumu sana. Naamini tunaweza kushinda kombe hili. Ni Kombe la Dunia, na linaweza kuja Congo”.

William Basimike, Bukavu, RFI Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *