Balozi na mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Katibu Mkuu na Rais wa Baraza la Usalama la umoja huo, akilaani mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Tehran na kutoa wito wa ufuatiliaji wa haraka na kutolewa ripoti rasmi kuhusu tukio hilo.

Amir Saeed Iravani amesema kwamba shambulio dhidi ya majengo ya Umoja wa Mataifa mjini Tehran ni ukiukaji wa wazi wa kinga ya shirika hilo la kimataifa.

Katika barua yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Iravani amesema: “Kwa kuzingatia majukumu uliyopewa Mheshimiwa kama kiongozi wa juu zaidi ya Umoja wa Mataifa, ni jukumu la lako kuhakikisha ulinzi na kinga ya majengo ya jumuiya hiyo katika nchi wanachama.”

Mwakilishi wa Iran Umoja wa Mataifa amesisitiza haja ya kushughulikia suala hilo rasmi kupitia mifumo husika ndani ya taasisi za Umoja wa Mataifa.

Amir Saeed Iravani ametoa wito kwa msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwasilisha ripoti kamili kwa nchi zote wanachama, ikiwa ni pamoja na maelezo kamili kuhusu mashambulizi dhidi ya vituo vya Umoja wa Mataifa, na kuchukua hatua na za haraka katika uwanja huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *