Hamis Mwinjuma maarufu kama @mwanafa , amesema serikali imetenga Sh400 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa matamasha na studio za kisasa za filamu nchini Tanzania.
Mwinjuma amesema hayo Aprili 2, 2026, bungeni mjini Dodoma akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga, kuhusu lini ujenzi wa mradi huo utaanza.
Alisema maandalizi ya mradi huo yapo katika hatua za mwisho, huku ujenzi ukitarajiwa kuanza hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha sekta za sanaa, utamaduni na michezo.
Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya msanii wa muziki wa Tanzania Diamond Platnumz @diamondplatnumz kueleza wasiwasi wake kuhusu ukosefu wa arena za kisasa kwa ajili ya sekta ya ubunifu nchini.
#kilichoborakabisa

(Feed generated with FetchRSS)