Chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimeuandikia Umoja wa Afrika, barua kupinga kuteuliwa kwa rais wa zamani Jakaya Kikwete, kama mjumbe maalum wa Umoja huo kwenye nchi za Pembe ya Afrika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

CHADEMA kinataka Umoja wa Afrika kufikiria tena hatua ya kumteua Kikwete kwenye nafasi hiyo, kwa kile chama hicho kinasema, ni kiongozi wa zamani anayeegemea upande mmoja kisiasa na mshirika wa karibu wa rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, barua hiyo inaeleza kuwa Kikwete hafai kwenye nagasi hiyo kwa sababu nchini Tanzania, amekuwa kikwazo kikubwa cha utekelezwaji wa katiba ya nchi hiyo.

Barua hiyo iliyoandikiwa na John Kitoka, Mkurugenzi wa masuala ya mambo ya nje na Diaspora kwenye chama hicho, imemshtumu Kikwete kwa kusalia kimya na kutolaani mauaji mabaya  na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyoshuhudiwa baada ya uchaguzi wa Oktoba tarehe 29 mwaka uliopita.

CHADEMA ambayo kiongozi wake Tundu Lissu bado yupo jela kwa tuhma za uhaini,  haijapokea majibu kutoka kwa Umoja wa Afrika, lakini  inasisitiza kuwa Kikwete sio chagua sahihi na hana sifa za kuwa mjumbe wa AU ambayo inasimamia misingi ya  kuheshimu haki za binadamu na utawala bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *