
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema nchi yake imepata mafanikio makubwa katika vita dhidi ya Iran, kufuatia mashambulizi ya pamoja na mshirika wake mkuu, Israel.
Katika hotuba kwa taifa iliyochukua takribani dakika ishirini, Trump amesema mashambulizi hayo, yaliyoanza mwezi mmoja uliopita, yamesababisha uharibifu mkubwa katika vituo vya urutubishaji wa nyuklia nchini Iran, pamoja na kuuawa kwa baadhi ya viongozi wa juu wa serikali hiyo.
Amesisitiza kuwa hatua hizo zimeudhoofisha kwa kiasi kikubwa uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Trump pia amesema kwa zaidi ya miaka 47, Iran imekuwa tishio kwa Marekani na nchi jirani, akitolea mfano jinsi mamlaka ya Tehran ilivyoshughulikia maandamano ya raia wake waliopinga utawala.
Rais huyo amesisitiza kuwa Marekani haitaruhusu Iran kumiliki silaha za nyuklia, akidai kuwa vituo vingi vya urutubishaji wa urani vimeharibiwa vibaya.
Soma zaidi: