MBUNGE wa Rorya, Jafari Chege amehoji Serikali kuhusu changamoto za utekelezaji wa mfumo wa manunuzi wa kielektroniki (NEST), licha ya mfumo huo kusaidia uwazi na usawa wa zabuni. Amesema baadhi ya watendaji wanajificha nyuma ya mfumo huo na kushindwa kutekeleza majukumu yao hali inayosababisha ucheleweshaji wa huduma na kukwamisha miradi ya maendeleo.

Kutokana na hali hiyo, ameitaka Serikali kuboresha mfumo huo ili kuongeza ufanisi. Aidha, ameitaka PPRA kutoa elimu kwa halmashauri kuhusu matumizi sahihi ya mfumo huo. Pia amesisitiza umuhimu wa utolewaji wa fedha za miradi kwa wakati na kuboreshwa kwa mifumo ya TEHAMA katika utoaji wa hati miliki za ardhi.SOMA: Matumizi mfumo NeST yaokoa bil 13.3/-

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *