Watu wawili waliofahamika kwa majina ya Said Saidi Ramadhani miaka 28 mkazi wa Mshangano na Lucas Gamaliel Mundo miaka 36 mkazi wa Mtyangimbole wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kutuhuma za muua dereva bodaboda baada ya kumteka na kumpeleka katika mji wa Peramiho kisha kumshambulia na kitu chenye nchi kali na kusababisha kifo chake hapo hapo .

Akitoa taarifa ya hali ya usalama na mafanikio yaliyopatikana kutoka na misako inayoendelea kwa waandishi wa habari kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma kamishna msaidizi mwandamizi Marco Chilya, amesema tukio hilo limetokea marchi 18 mwaka huu majira ya usiku..

Katika tukio nyingine Jeshi la Polisi linamshikilia Micheal Ngonyani miaka 38 mkazi wa Kijiji cha Mtyangimbole kwa kujihusisha na uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo wizi wa magari na vitu vya majumbani mkoani Mbeya.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *