Mamlaka ya Dawa, Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Kanda ya Magharibi, imetoa elimu kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mafunzo hayo yamehusu utambuzi wa madhara na matukio yanayotokana na matumizi ya vifaa tiba ikiwa ni sehemu ya jitihada za kulinda usalama wa jamii.

Washiriki hao wamepata fursa ya kujifunza namna ya kubaini mapema changamoto zinazojitokeza katika matumizi ya vifaa tiba pamoja na hatua stahiki za kuchukua.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Magharibi, Kiboko Pascal amesema lengo la mafunzo hayo unayofanyika katika Kituo cha Macren ni kuwajengea uwezo watoa huduma za afya Ili watambue madhara yanayosababishwa na vifaa visivyo salama na vinavyoharibika.

Ameongea kuwa watoa huduma wameelekezwa namna sahihi ya kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapobaini kasoro katika vifaa tiba hatua ambayo ni muhimu katika kuchukua tahadhari za haraka na kuzuia madhara zaidi kwa wagonjwa.

*Imeandaliwa na Caren-Tausi Mbowe*

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *