Ndege mbili za kivita za Marekani zimedondoshwa kutoka juu ya anga ya Iran. Mmoja wa marubani anatafutwa kwa na Marekani na Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti siku ya Ijumaa kwamba mmoja wa marubani wa ndege hizo mbili za Marekani zilizoangushwa aliokolewa kusini-magharibi mwa Iran. Hatima ya rubani wa pili, ambaye bado anatafutwa kwa , bado haijulikani.

Israel imesitisha mashambulizi nchini Iran

Afisa wa Israel ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba Israel imesitisha mashambulizi yake ya anga nchini Iran kama sehemu ya shughuli za utafutaji na uokoaji za Marekani.

Iran yadai kudondosha ndege ya Marekani A-10

Ndege ya Marekani A-10 ilipigwa na ulinzi wa anga wa Iran, vyombo vya habari vya serikali ya Iran viliripoti, vikinukuu ofisi ya uhusiano wa umma ya jeshi la Iran. Hapo awali shirika la hbari la Associated Press liliripoti kwamba ndege ya pili ya kivita ya Jeshi la Anga la Marekani ilianguka Mashariki ya Kati siku ya Ijumaa.

Hakuna taarifa zaidi zilizopatikana mara moja, ikiwa ni pamoja na mahali rubani alipo. Pentagon na Ikulu ya White House hawawajazungumza chochote. Ndege aina ya A-10, ambayo pia inajulikana kama Warthog, ni ndege ya kiti kimoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *