Mlipuko mkubwa umesikika Ijumaa, Aprili 3, 2026, huko Khartoum, mji mkuu unaodhibitiwa na jeshi la Sudan, kulingana na mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP na mashahidi.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wa habari wa AFP huko Omdurman, mji ulio karibu na Khartoum upande wa pili wa Nile, alisikia mlipuko huo ukitoka katikati ya mji mkuu, huku shahidi katikati ya jiji akielezea “mlipuko mmoja mkubwa” na kuongeza kuwa hakuona dalili zozote za moto au moshi.

Mamlaka haijazungumza chochote kuhusu mlipuko huo, ambao unakuja baada ya miaka mitatu ya vita kati ya jeshi la Sudan na wanajeshi wa Vikosivya Usaidizi wa Haraka (RSF).

Polisi wa Sudan wamethibitisha mlipuko katika wilaya ya Burri mashariki mwa Khartoum, karibu na maeneo kadhaa ya kimkakati ikiwemo makao makuu ya jeshi na uwanja wa ndege wa kimataifa wa jiji hilo. Walisema kwamba ulisababishwa na omu la ardhini lililolipuka baada ya “baadhi ya wakazi kuchoma takataka,” na kwamba hakukuwa na majeruhi.

Khartoum “imechafuliwa na vifaa ambavyo havikulipuka” Mlipuko huu unakuja baada ya miaka mitatu ya vita kati ya jeshi la Sudan na wanajeshi wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF). Mgogoro huo, kati ya Jenerali al-Burhan na msaidizi wake wa zamani Jenerali Mohamed Daglo, mkuu wa RSF, tayari umesababisha makumi ya maelfu ya watu kupoteza maisha na kusababisha zaidi ya watu milioni 11 kutoroka makazi yao. Katika miezi iliyofuata jeshi kuiteka tena Khartoum mwezi Machi mwaka jana, RSF ilishambulia kambi za kijeshi na miundombinu ya raia katika mji mkuu kwa kutumia ndege zisizo na rubani. Lakini hakukuwa na mashambulizi ya anga katika miezi ya hivi karibuni, na hali imerejea katika hali ya kawaida.

Hivi majuzi Umoja wa Mataifa ulionya kwamba Khartoum bado “imechafuliwa sana na silaha ambazo hazijalipuka,” ikibainisha kuwa mabomu yamegunduliwa kote jijini. Mengi ya mabomu haya yaliachwa nyuma na wapiganaji wa RSF, ambao waliteka udhibiti wa jiji hilo katika siku za mwanzo za vita.

Mgogoro huo hivi karibuni umeenea katika maeneo mapya, ikiwa ni pamoja na maeneo ya kusini ya Kordofan na Blue Nile. Juhudi za kukomesha vita, zikiongozwa na Marekani, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, na Misri, zimeshindwa hadi sasa, kwani pande zote mbili zinatiwa moyo na mafanikio yaliyopatikana katika uwanja wa vita katika maeneo mbaimbali. Kulingana na wachambuzi, hali hiyo inazidi kuwa ngumu kutokana na kwamba Jenerali al-Burhan anategemea mitandao ya Kiislamu ambayo inaogopa kuwa makubaliano ya amani yanaweza kuwatenga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *