Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limewakamata watuhumiwa 25 kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la mauaji ya Henry Shubati Myuwanga ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Wema Mkoani Songwe.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Shadrack Masija, amesema tukio hilo lilitokea jana usiku katika Kijiji cha Kilyamatundu, Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa baada ya mwalimu huyo kufika kijijini hapo akitokea Mlowo Mkoa wa Songwe kwa lengo la kuuza sabuni za maji anazotengeneza.

Kwa mujibu wa Kamanda Masija chanzo cha tukio hilo kilitokana na kutokukubaliana bei ya sabuni kati ya mwalimu huyo na kijana mmoja muuza duka kijijini hapo aitwaye Clement Simchimba ambaye kwa sababu zake anazojua aliamua kupiga kelele na kumtuhumu marehemu kuwa amemshika bega na kwamba nyeti zake zimepotea.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *