Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), imesema hakuna dawa zilizowekwa misumari na kwamba taarifa hizo ni za uzushi.
Kwa mujibu Mamlaka hayo, video zinazoonyeshwa kuna misumali ndani ya baadhi ya dawa zimeandaliwa kwa lengo la kupotosha na kuzua hofu kwa jamii.
“Kufungua sampuli na kuweka vitu vya kigeni ni mbinu inayotumiwa na watu wasio waaminifu kutengeneza maudhuhi ya kushtusha,” imesema taarifa hiyo iljyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, dawa zote zinazoingia nchini ukaguliwa na Mamlaka hayo na kwamba viwanda vyote vina mifumo ya mashine inayozalisha maelfu ya vidonge kwa dakika na haiwezekani kwa msumari mmoja mmoja kuingizwa ndani ya kapsuli moja.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa,.endapo kungekuwa na kitu kigumu kama msumari ndani ya kapsuli mashine hizo zingeharibika na hata kushindwa kufunga kidonge vizuri.
Mamlaka hayo imewataka wananchi wanapohisi au kuona kitu kisicho cha kawaida wasikimbilie katika mitandao na badala yake watoe taarifa kwao Ili zifanyiws kazi haraka.
Imeandaliwa na Caren-Tausi Mbowe
#startvupdate
(Feed generated with FetchRSS)