Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetumia Sh30 milioni kusaidia jamii isiyojiweza. mkoani Songwe.

Fedha hizo.zimetumika kununua dawa mbalimbali kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe lengo ikiwa ni kurudisha kwa jamii.

Msaada huo umetolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Songwe, Kituo cha Afya cha Tunduma
na Hospitali ya Wilaya ya Mbozi ili kupunguza changamoto ya upungufu wa dawa katka vituo hivyo.

Meneja wa TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Anitha Mashighati amesema msaada huo umelenga kuwafkia wananchi wenye uhitaji mkubwa ambao wanashindwa kumudu gharama za matibabu hususani ununuzi wa dawa muhimu

Kwa mujibu wa meneja huyo, TMDA imeona ni muhimu kurudisha kwa jamii kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya Ili kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wote bila kujali hali zao za kiuchumi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *