Vyanzo vya kijeshi nchini Sudan, vinadai kuwa zaidi ya mamluki wa kigeni 850 wanapigana sambamba na vikosi vya RSF, ripoti inayothibitisha namna utegemezi wa wapiganaji wa makampuni binafsi na makundi mengine ya kikanda unaongezeka.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo hivyo vimesema mamluki hao wanajumuisha wanajeshi wa zamani pamoja na wataalam wenye tajiriba katika masuala ya kivita.

Ripoti inajiri baada ya baraza la usalama katika Umoja wa Mataifa mwezi Januari kuonya kwamba vita vya Sudan huenda vimeingiliwa na nguvu za kigeni.

Kulingana na baraza hilo, uwepo wa nguvu kutoka nje unatishia kuyumbisha zaidi eneo la Sahel na baadhi ya maeneo katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mwaka uliopita, Ofisi ya  Rais wa Colombia ilithibitisha kuwa karibia raia wake 40 waliuawa katika shambulio kwenye uwanja wa ndege wa Nyala jijini Dafur.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *