Chama cha Kudhibiti Tumbaku Tanzania kimeiomba Serikali na wadau kuhakikisha kuwa muswada wa sheria ya kudhibiti matumizi ya tumbaku unapelekwa bungeni ili kuokoa wananchi wanaopata madhara makubwa kutokana na uvutaji wa tumbaku.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Tumbaku Tanzania, Dkt Lutgard Kagaruki wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Tobacco Industry Interference Index 2025, inayoangazia jinsi makampuni ya tumbaku yanavyoingilia Sera za Afya za nchini.
“Serikali ichukue hatua kuharakisha mabadiliko ya sheria za kudhibiti matumizi ya tumbaku na kusisitiza kuwa lengo si kuzuia kabisa uuzaji wa sigara, bali kuhakikisha zinatumika kwa tahadhari kubwa kupitia sheria kali zitakazopunguza matumizi holela.
Matumizi ya tumbaku yamekuwa kichocheo kikubwa cha kuomgezeka kwa maradhi ya kansa ambako Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) ina jukumu la kudhibiti bidhaa hizo kwa usimamia ubora na usalama wa bidhaa zinazoweza kuathiri afya ya binadamu, ikiwamo,
bidhhaa za tumbaku kwa upande wa usalama na viwango vya kemikali.
Pia TMDA inajukumu la kudhibiti matangazo na maudhui ya bidhaa hizo hasa yanayohusiana na afya, pamoja na kutoa au kukagua vibali vya baadhi ya bidhaa zinazohusiana na matumizi ya binadamu.
#StarTvUpdate
(Feed generated with FetchRSS)