
Karibu miaka miwili baada ya kukamatwa kwake huko Zémio, kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, mtafiti, raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Ureno na mtetezi wa haki za kibinadamu Joseph Figueira ameachiliwa, baada ya kukamatwa kwa “kuhatarisha usalama nchi,” ameondoka Bangui siku ya Jumanne, Aprili 7.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hii inaashiria mwisho wa karibu miaka miwili ya hali nzito kwa Joseph Figueira. Alikamatwa mwishoni mwa mwezi Mei 2024 na wanamgambo wa Urusi wa kundi la Wagner huko Zémio, ambapo alikuwa akifanya kazi kwa shirika lisilo la kiserikali la Marekani la FHI 360, alihukumiwa mnamo mwezi Novemba 2025 kifungo cha miaka kumi ya kazi ya kulazimishwa, haswa kwa “kuhatarisha usalama wa taifa.” Alikuwa akikanusha tuhuma za kushirikiana na makundi ya waasi. Upande wake wa utetezi ulishutumu kesi ” ya kisiasa” na “isiyo ya haki”.
Kukamatwa kwake kuliambatana na kampeni ya uhusiano wa umma na mitandao ya Urusi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikimwonyesha kama jasusi wa Marekani mwenye uhusiano na makundi ya waasi, ikiwa ni pamoja na LRA na UPC.
Siku ya Jumanne, Aprili 7, aliondoka kwa siri katika chumba ambako alikuwa akizuiliwa Camp Roux, ambapo alishikiliwa kwa zaidi ya miezi 22. Mtafiti huyo mwenye uzoefu na mtetezi wa kibinadamu, mtaalamu wa masuala ya watu kutoka jamii ya Fulani na mabadiliko ya ubinadamu, Joseph Figueira alipanda ndege ya kijeshi kwenda Lisbon, ambapo aliunganishwa tena na familia yake. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno, Paulo Rangel, ndiye alitangaza kuachiliwa kwake wakati wa kikao cha bunge siku ya Jumanne alasiri.
Juhudi za kidiplomasia zilizoimarishwa
Kuachiliwa huku kunakuja wiki moja baada ya kuanza rasmi kwa muhula wa tatu wa Rais Faustin-Archange Touadéra. Vyanzo kadhaa vinaona kama ishara kwa Umoja wa Ulaya, mfadhili mkuu wa nchi hiyo. Kuachiliwa kwake kulitakiwa mara mbili na maazimio ya Bunge la Ulaya. Kuachiliwa huku kunakuja baada ya juhudi za kidiplomasia zilizoimarishwa na Ureno, nchi inayohusika sana na Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikiwa na wanajeshi zaidi ya 200 waliowekwa ndani ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa, MINUSCA.
Mwishoni mwa mwezi Februari, Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa alizuru Bangui katika siku za mwisho za muhula wake. Kulingana na vyanzo kadhaa, alikasirika kuondoka bila ya kuachiliwa kwa raia huyo. Jukumu hili lilichukuliwa na mrithi wake, António José Seguro.
Kulingana na tovuti ya Africa Intelligence, kumekuwa na mawasiliano ya simu karibu kila siku na Rais Touadéra tangu mwisho wa wiki iliyopita.