Mamlaka nchini Tanzania zimetangaza kuongeza muda zaidi wa siku 21 kwa tume maalumu inayochunguza vurugu za wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Octoba mwaka uliopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia gazeti la Serikali na kusainiwa na mwenyekiti wa tume hiyo jaji mstaafu Mohammed Chande Othman, hatua hii ilifuatia ombi lao la kutaka siku zaidi ili kukamilisha hatua muhimu za uchunguzi wao.

Aidha nyongeza hii ya siku inalenga kuipa nafasi tume kuchambua Ushahidi, taarifa na maoni iliyoyapokea wakati wa mahojiano iliyoyafanya na wadau mbalimbali.

Polisi wa Tanzania wakimvuta mtu wakati wa maandamano kwenye eneo la Namanga mpaka na Kenya.
Polisi wa Tanzania wakimvuta mtu wakati wa maandamano kwenye eneo la Namanga mpaka na Kenya. REUTERS – Thomas Mukoya

Wakati tume hiyo ikiongezewa muda mwezi Februari, ilisema kulitokana na kujitokeza kwa idadi kubwa zaidi ya watu kuliko walivyotarajia kutaka kutoa ushirikiano na tume hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa tume hii kuongezewa muda,  ambapo wakati ikitangazwa kuanza kufanya kazi Novemba 20 mwaka uliopita, ilipewa siku 90 na baadae kuongezewa siku 42 ambazo zilitamatika April 3, na sasa nyongeza wa siku 21 ikitarajiwa kumalizika April 24 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *