Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro limemkamata Abdul Mongola (24) mkazi wa Saba saba Mkoani hapo dereva boda boda kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuwa ameibiwa nyeti zake.
Mtuhumiwa huyo akiwa anafanya shughuli zake za boda boda sehem za nane nane aliitwa na abiria ambae jina lake limehifadhiwa aliitwa na Abiria ampelekea mjini kati na baada ya kumbeba aligundua kushikwa katika bega lake ndio na kuamua kuendesha piki piki yake hadi nane nane na kusema ameibiwa nyeti zake.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro RPC Andrew Kantimbo amesema uchaguzi wa awali uliofaywa na madaktari wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro umebaini kuwa mtuhumiwa huyo hajaibiwa nyeti zake na alifanya hivyo kwa lengo lake maalumu ambalo bado wanachunguza.
(Feed generated with FetchRSS)