
Gambia imemteua mwendesha mashtaka maalumu ikiwa ni karibu miaka miwili tangu ilipotangaza kuunda nafasi hiyo kwa ajili ya kuendesha kesi za uhalifu uliotekelezwa wakati wa utawala wa kikatili wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo,Yahya Jammeh.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wizara ya sheria ilitangaza kuwa imemteua wakili raia wa Uingereza, Martin Hackett, kusimamia ofisi hiyo, rekodi yake ikihusisha kazi alizofanya kushughulikia makosa ya uhalifu wa kivita, mauaji ya kimbari na ugaidi.
Uteuzi wake umekuja wakati ambapo serikali imekuwa ikikosolewa kwa kasi ndogo ya kuteua na kushughulikia kesi za uhalifu uliotekelezwa chini ya utawala wa Jammeh.
Mwezi April mwaka 2014, bunge la Gambia lilipitisha sheria iliyoanzisha ofisi maaluùu ya mwendesha mashtaka kushughulikia kesi zilizobainishwa na tume ya ukweli na maridhiano.
Wakati wa utawala wa Jammeh kuanzia mwaka 1994 hadi 2017, watu kati ya 240 na 250 waliuawa na vyombo vya usalama, hii ni kwa mujibu wa tume ya ukweli na maridhiano, ambayo pia ilipata ushahidi wa vitendo vya mateso, utekaji, ushirikina na unyanyasaji mwingine.