
Mahakama ya Rufaa ya Rabat nchini Morcco imethibitisha Jumatatu jioni, Aprili 13, 2026, hukumu zilizotolewa na mahakama ya mwanzo katika kesi dhidi ya wafuasi 18 wa timu ya taifa ya soka ya Senegal walioshtakiwa kwa vurugu wakati wa fainali ya AFCON: tisa kati yao wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela, sita wamehukumiwa kifungo cha miezi sita, na watatu wanaosalia wataweza kurudi nchini mwao baada ya siku chache.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Morocco, Matthias Raynal
Baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela, hivi karibuni mashabiki watatu wa timu ya taifa ya soka ya Senegal watakuwa wametumikia kifungo chao.
Mawakili wa upande wa utetezi, mawakili wa vyama vya kiraia, na mwendesha mashtaka kila mmoja alipewa nafasi ya kuzungumza, huku hoja za mwisho na zikifuatana katika kikao hiki kilichodumu kwa saa tisa. Upande wa utetezi unaibua makosa ya kiutaratibu na kuomba mwakilishi wa CAF ahojiwe wakati wa kesi. Hatimaye mahakama iliamua kushughulikia masuala haya wakati wa uamuzi.
Washtakiwa ambao ni mashabiki wa timu ya taifa ya soka ya Senegal walihojiwa tena na mahakama, mmoja baada ya mwingine, ili kutoa toleo lao la matukio. Wote walikana kushiriki katika vurugu hizo. Baadhi walisema walishuka kwenye uwanja wa Moulay-Abdellah ili kuepuka umati wa watu waliokuwa kwenye vibanda.
Muda mfupi baada ya saa 4 usiku, Mahakama ya Rufaa ya Rabat (kaskazini magharibi mwa Morocco) ilikutana katika faragha ili kuchukuwa maamuzi. Saa moja baadaye, uamuzi ulitolewa; hukumu zilizotolewa zilikuwa sawa na zile za awali.