
Kwa bei za chini kabisa za umeme Afrika Mashariki, soko la magari ya umeme linaanza kushika kasi kubwa nchini Tanzania. Fursa hii imechukuliwa na JTP, moja ya kampuni za kwanza kutoa magari ya umeme 100%, kwa lengo la kufanya usafiri kuwa wa kijani zaidi huku ikipunguza gharama.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mbali na hoja ya mazingira, ni juu ya gharama zake zote za uendeshaji zinazovutia. “Ikilinganishwa na lori la kawaida, pamoja na mgogoro wa mafuta na bei za sasa, tunaokoa hadi 90% kwa gharama kwa kila kilomita,” anasema Amar Shangavi, mkurugenzi na mwanzilishi wa JTP.
Chaji kamili hugharimu takriban euro 4 kwa umbali wa kilomita 250. Kwa kulinganisha, huku lita moja ya petroli ikigharimu euro 1.25 jijini Dar es Salaam, kusafiri umbali huo huo kungegharimu zaidi ya euro 28 kwa gari la injini ya mwako, mashine inayozalisha nguvu kwa kuchoma mafuta (petroli au dizeli) .
JTP inatoa aina mbalimbali, kuanzia magari madogo hadi magari ya kubeba mizigo, yote yakiagizwa kutoka China. “Soko la China kwa sasa limejaa. Kwa hivyo, makampuni ya kutengeneza magari ya aina hiyo wanatafuta kuuza nje, na Afrika iko katika nafasi nzuri ya kufaidika na bei hizi za ushindani,” anaelezea Amar Shangavi.
Miundombinu bado midogo
Bei za kuvutia, lakini pia utaalamu unaotambuliwa katika magari ya umeme: hizi ni hoja zilizomshawishi Matthew Haden, mwanzilishi wa kampuni ya kuchakata ya The Recycler, mmoja wa wateja wa kwanza wa JTP. Lakini maswali yamekosa majibu: “Tanzania si China. Tuna mvua nyingi, barabara zilizoharibika … Tunahitaji kuona jinsi magari yanavyoendelea hapa, na zaidi ya yote, jinsi ya kupata vipuri na kuhakikisha matengenezo yanafanywa haraka.”
Kikwazo kingine kikubwa: mtandao wa kuchaji, ambao bado ni changa. Nchi ya Tanzania ina vituo vya kuchaji takriban kumi na tano pekee, hasa katika miji mikubwa, na kukatika kwa umeme ni changamoto nyingine.
“Kwa sasa tunaendeleza vituo vya kuchaji jijini Dar es Salaam. Lengo ni kuwezesha kuchaji haraka, hata wakati wa kukatika kwa umeme usiku,” anasema Amar Shangavi. Serikali ya Tanzania inalenga vituo 500 vya kuchaji ifikapo mwaka 2030.
Kwa zaidi ya 60% ya umeme wake unatoka kwenye vyanzo mbadala, Tanzania ina nafasi kubwa ya kusaidia mabadiliko haya.