Mazungumzo kati ya Marekani na Iran yanaweza kuanza tena “katika siku mbili zijazo,” Donald Trump ameliambia Gazeti la New York Post. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

“Jambo linaweza kutokea katika siku mbili zijazo, na tutakuwa na mwelekeo zaidi wa kwenda Pakistan,” ameliambia gazeti hilo.

Taarifa hii inakuja baada ya mkutano uliofanyika mwishoi mwa wiki iliyopita huko Islamabad, Pakistan, uliohudhuriwa, miongoni mwa wengine, Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance na Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf. Mazungumzo hayo yalimalizika bila makubaliano yoote.

Mapema siku hiyo, vyombo vya habari vya serikali ya Iran viliripoti kubadilishana ujumbe kati ya Tehran na Pakistan, lakini vikabainisha kwamba hakukuwa na “taarifa” inayoonyesha makubaliano ya kufanyika kwa mazungumzo mapya na Marekani.

Licha ya matumaini ya kurejea mazungumzo, Washington imeapa kuendelea na shinikizo dhidi ya Iran.

Wizara ya Fedha ya nchi hiyo imesema haina mpango wa kulegeza tena vikwazo kwa biashara ya mafuta ya Iran baada ya hapo kabla kuruhusu mauzo ya mafuta ya nchi hiyo kufidia upungufu uliojitokeza baada ya kuzuka vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *