Hali mashariki mwa DRC iko kwenye ajenda ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, Aprili 15, jijini New York. Kwa kutarajia mkutano huu, Human Rights Watch imechapisha ripoti inayoangazia ugumu unaowakabili raia katika mkoa wa Kivu Kusini, haswa katika eneo la vilima ambapo mapigano mengi yamejikita katika wiki za hivi karibuni. Shirika la haki za binadamu linaamini kwamba kwa sasa, “pande zote zinazopigana zinatishia misaada ya kibinadamu na ulinzi wa raia.”

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Raia wako njia panda hawajui la kufanya wala pakwenda,” anaelezea Clémentine de Montjoye, mtafiti mkuu katika eneo la Maziwa Makuu katika shirika la Human Rights Watch. “Wanakabiliwa na unyanyasaji kutoka pande zote.” “Kwa upande mmoja, Twirwaneho [wanamgambo washirika wa M23] katika maeneo wanayodhibiti wamewatishia na kuwaajiri raia kwa nguvu na pia wanawazuia raia kuondoka Minembwe licha ya mapigano yanayoendelea katika eneo hilo. Kwa upande mwingine, watu tuliowahoji walituambia pia wanahofia dhuluma, haswa na makundi ya Wazalendo, ambayo yanashirikiana na jeshi la Kongo na ambayo, katika maeneo yanayodhibitiwa na makundi haya, yameweka vizuizi vya barabarani, wamewanyanyasa watu, au hata kuwaweka kizuizini baadhi ya watu katika vituo visivyo rasmi vya kizuizini,” mtafiti ameongeza.

“Kwa hivyo, ujumbe tulionao leo ni kwamba lazima tusisitize na kuweka shinikizo kwa pande mbalimbali kwenye mzozo ili kurahisisha ufikiaji wa kibinadamu na kuheshimu kanuni za msingi za sheria ya kimataifa ya kibinadamu kuhusu ulinzi wa raia.” Hii ni kwa ajili “kuwaruhusu raia kukimbia mapigano kwa salama.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *