serikali kupitia TARURA kuzingatia zaidi ujenzi wa mitaro ili kulinda miundombinu ya barabara badala ya kufanya ukarabati wa mara kwa mara.
Amesema endapo mitaro ya kutosha itajengwa pamoja na makaravati na madaraja, barabara nyingi zitakuwa imara hata wakati wa mvua kubwa.
Mgore ameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza uharibifu wa barabara unaotokea kila msimu wa mvua.
Ameongeza kuwa fedha nyingi za serikali zinazotumika kufanya matengenezo ya mara kwa mara zinaweza kuokoa na kuelekezwa kwenye miradi mingine ya maendeleo.
Mbunge huyo ametoa ushauri huo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka wa fedha 2026/2027.
(Feed generated with FetchRSS)